ELIMU NA KILIMO,BUNGOMA

ELIMU NA UCHUMI,WEBUYE MAGHARIBI.
Tarehe 3 Mei 2024
Wito umetolewa kwa wanafunzi kujitenga na  visa vya tabia potovu ambazo zinaweza sababisha maisha yao kuzorota.
Haya ni kwa mujibu wake mwalimu mkuu wa shule ya upili ya wasichana ya Lugulu Bi Dinah Cheruyoit kwenye hafla ya changisho iliyoandaliwa katika shule ya upili ya mtakatifu Anne Maloho wadi ya Bokoli-Webuye Magharibi.
Cheruyoit aliyekuwa mgeni wa heshima katika hafla hiyo,alitumia fursa hiyo kuwataka wanafunzi kukomesha uhusiano wa mapenzi wakiwa wangali shuleni kama njia mojawapo ya kuzuia visa vya mimba za mapema.Aidha alisisitiza kuwepo haja ya wazazi kuwajibika kuendeleza elimu ya wanao katika vitengo mbalimbali baada ya kumaliza vidato vya nne ili kuwawezesha kujimudu mbeleni.
"Kama uko na mtoto nyumbani hakufaulu kuingia chuo kikuu,wacha waingie vyule vya kiufundi vyenye serkali imeleta zenye zinawapa mpaka mikopo,hakuna kuhangaika wacha watoto wapate ujuzi na wajiunge na vikundi wajisajili serkali itawasaidia", Kauli yake bi Cheruyoit.(Kauli ya Sauti iliyonaswa ipo).

Bi Cheruyoit akiendeleza changisho-mpiga picha Sakwa.

Cheruyoit kwenye sekta ya uchumi wa nchi,aliwarai wakaazi kujiunga na upanzi wa avokado huku akihoji uzalishaji wa matunda hayo ni wa dhamana kwa kuleta pesa haraka mifukoni mwa watu.
Hafla hii pia ilihudhuriwa na mwakilishi wadi wa Bokoli Jack Kawa,aliyetumia fursa hiyo kutoa tahadhari kwa wahusika wa kunyemelea watoto wasichana wa shule pamoja na wanafunzi wanaojiingiza katika uhusiano wa kimapenzi kuwa mkono wa sheria uko tayari kukabiliana nao kuwa ndio chanzo cha kusababisha visa vya mimba za mapema.

        Kawa,kwenye changisho-Mpiga picha Sakwa

Zaidi ya ksh.laki nne(400,000) zilichangwa katika hafla hii.
       Uchapisho wake,
       Simiyu Sakwa,
        Webuye Magharibi

Comments

Popular posts from this blog

UKATILI,BOKOLI-WEBUYE MAGHARIBI.

BUKUSU CULTURAL CENTRE

KUMWONJOLOLI KWE LIMENYA LIA KUKHU DINAH NAFULA MANYONGE.