HISTORIA YA MAREHEMU ZAKAYO MILIMO TUMWA.
1.KUZALIWA
Marehemu Zakayo alizaliwa mwaka wa 1982 akiwa mtoto wa pili wa Silas Tumwa(Mutecho)na Everlyne Nafula(Muliuli).

KANISA
Mwendazake Zake Zakayo Milimo alipokelewa katika matabau ya kanisa la marafiki mwaka wa 1984.

ELIMU
Mwenda zake Zakayo Milimo alianza elimu yake katika darasa la kwanza katika shule ya msingi ya Kitale stesheni mwaka wa 1987 hadi darasa la pili.
1994 alijiunga na shule ya msingi ya Bokoli Rc katika darasa la tatu na kusoma hadi darasa la name na kufanya mtihani wa kitaifa KCPE na kupita vizuri.
Mwaka wa 2000 alijiunga na shule ya upili ya marafiki ya Mahanga katika kidato cha kwanza Hadi 2003 katika kidato cha tatu.
Mwaka 2004  alijiunga na shule ya upili ya mtakatifu Maria-Bokoli katika kidato cha nne ambapo alikalia mtihani wa kitaifa wa sekondari KCSE.
2006 Alijiunga na taasisi ya kiufundi ya Matili na kusomea Ujenzi.

TOHARI
Marehemu alipaswa tohara mwaka wa 1996 akiwa Omusawa nambari 5.

KAZI
Mwenda zake aliajiriwa kuuza katika Duka maeneo ya Gilgil,kaunti ya Nakuru mwaka 2007.
2008 aliweza kuajiriwa katika Kampuni ya kutengeneza Unga ya Kitale.

NDOA
Marehemu alibarikiwa Ndoa yake kutoka Kwa ukoo wa Balisa,mwaka 2008.
Aliweza kupata mtoto wa kiume na mama Biliya Mulongo mwaka wa 2018.

UGONJWA.
Alizaliwa na afya njema hadi mwezi wa Saba mwaka wa 2004 aliweza kuhisi maumivu ya viungo vya mwili,aliweza kuhudumiwa katika hospitali ya Bokoli alipogunduliwa kuwa na Malaria.
Mwezi wa 10,2024 alipatwa na ugojwa wa macho kupoovuka.
15/10/2024,alipelekwa katika hospitali ya rufaa ya Bungoma,ambapo vipimo vitatu vilifanyika na kubaini kuwa Maini ilikuwa na  uvimbe hali inayosababisha maji kumwagika mwilini.Aliweza kutibiwa chini ya Daktari Marko kutoka hospital ya Bumula.
5/1/2025,alihisi maumivu ya tumbo tena,aliweza kupelekwa Kwa matibabu ili ukarabati wa kupunguza maji mwilini kutekelezwa.
Mwishoni mwa mwezi wa Februari 2025,aliweza kuvurutwa maji mwilini katika hospitali ya kibinafsi ya Nzoia Medical centre-Chwele,baada ya Daktari Marko kupata Kazi nyingine nchini Uganda.
6/3/2025,alizidiwa na maumivu ya tumbo,Hali iliyosababishwa kupelekwa katika hospitali ya kimisheni ya Chebukaka.Alitibiwa na kurudi Kwa Nduguye Oliver-Chekwanda.
7/3/2025,Hali ilizidi kugeuka na kuwa mbaya,Hali iliyofanya kupelekwa katika hospitali ya rufaa ya Bungoma.Aliweza kulazwa Kwa siku tatu na kufuatia ulekevu wa Madaktari,hali Yake ilizidi kuwa mbaya zaidi na kusababisha kifo chake siku ya Jumatatu 9/3/2025.
Marehemu ameaga dunia na umri wa miaka 43,ameacha nyuma mtoto mmoja mvulana


RATIBA YA MAZISHI YA ZAKAYO MILIMO
1.OMUTECHO
2.OMUTILU
3.OMULIULI
4.WAJOMBA
5.WAKWE
6.MASHANGAZI
7.WAZAZI
8.MWENYEKITI WA UKOO
9.JIRANI
10.WANAKANDANDA
11.HISTORIA-REDIO
12.KAMATI YA MAZISHI
13.UTAWALA
14.KANISA

Comments

Popular posts from this blog

UKATILI,BOKOLI-WEBUYE MAGHARIBI.

BUKUSU CULTURAL CENTRE

BUNGOMA,HEALTH UPDATES