WANAWAKE UONGOZINI

FANAKA UONGOZINI NA WANAWAKE.
Huku mirindimo ya kisiasa ya kubaini wamiliki wa nyadhifa mbalimbali uongozini kwenye uchaguzi wa 2027,ni jukumu la kila mkenya kuwa  tayari kuchagua kiongozi bora na si bora kiongozi.
Katiba ya Kenya kusisitiza kuwepo kwa usawa wa jinsia,ni nafasi tendeki kwa wanawake pia kujiingiza kwenye kinyang'anyiro cha kuwania nafasi uongozini.
Usawa wa jinsia kuungwa mkono,wanawake wamejipata katika nyanja mbalimbali uongozini ikiwemo uwakilishi wadi,ubunge,uwakilishi wa kina mama,useneta na Ugavana.Hii ni  ramani kuwa hakuna kizuisi cha  kumpinga mwanamke yeyote kwenye tajariba  ya kukomboa taifa katika nafasi yeyote ya uongozi wa nchi.
Jaji Martha koome kuwa rais wa kwanza mwanamke wa mahakama ni changamoto kubwa kwa mtoto msichani kuwa na picha ya uwezekano katika pilika za kusimamia kitengo au nafasi fulani anapokubaliwa na wanainchi.
       Jaji mkuu Bi.Martha Koome
Katika serkali za Ugatuzi na hata ngazi za juu,ipo haja ya kutambua kuwa wanawake wanayo tajiriba pia ya kuongoza iwapo wanaweza pata nafasi hizo.
Tarubini ya MBUkusuTV,inaangazia uongozi wa kaunti 7 humu nchini ambazo zinaongozwa na wanawake,Wavinya Ndeti-Machakos,Glady's Wanga-Homabay,Anne Waiguru-Kirinyaga,Kawira Mwangaza-Meru,Cecily Mbarire-Embu,Susan Kihika-Nakuru na Fatuma Achani wa kwale.Ni wanawake ambao wameandikisha rekodi ya kutambua kuwa yawezekana pia kuongoza magatuzi.
    Gavana wa Machakosi Vavinya Ndeti akiwarai wanawake kuwania nyadhifa uongozini.
Twasira ya leo ni kulega mkoa wa magharibi ambao unajumulisha kaunti tano; Kakamega,Bungoma,Busia,Vihiga na Trans Nzoia.Je, Kaunti hizi zimewahi 
wapea wanawake kibau mbele kwenye kinyang'anyiro cha Ugavana?
  Gavana wa Kirinyaga-Anne Waiguru
Basi ni Jukumu la wanawake kutoka gatuzi hizi pia kujiamini na kujiingiza katika nafasi za kuwaomba wanainchi kuchaguliwa hata katika nyadhifa za Ugavana na si tu nafasi za unaibu wa ugavana.
Uchapisho wake,
Simiyu Sakwa,Bungoma.

Comments

Popular posts from this blog

BUNGOMA,HEALTH UPDATES

BUKUSU CULTURAL CENTRE

WANAMEME RECOGNIZED BY STATE