UONGOZI NA ELIMU HITAJIKA
BUNGOMA:
Makanisa yamehitajika kuwa kielelezo cha kukosoa maovu humu nchini ili kuweka taifa kwa ustaarabu wa utendakazi kutoka kwa serikali.Ni Kauli yake kamishna Jack Tumwa akihotubia waombolezaji kwenye hafla ya mazishi katika kijiji cha makunda,kata ya Bokoli Magharibi mwa Webuye.
Tumwa ambaye amewahi hudumu kama mmoja wa makamishna wa tume ya zamani ya uchaguzi humu nchini ECK,amesema madhehemu yanatakikana kuwa wazi kukosoa serikali pasipo na uoga kufwatia hali ngumu ya maisha ambayo wakenya wanapitia kwa sasa.
"Wenzangu wakristu,sisi tunazama hatukuji kuambia watu kinachotendeka kwa kuhofia tusichokijua,hili taifa ni lazima zote tuamke tuseme hatuendi kwa mkondo mzuri tuliombee taifa hili ndio maana wanaotuongoza watatusaidia turekebishe panapohitajika", asema ambassador Tumwa.
.......kauli ya sauti iliyonaswa ipo........
Haya yamesungumziwa katika hafla ya mazishi katika kijiji cha Makunda-Kata ya Bokoli Eneo bunge la Webuye Magharibi.
Mwakilishi wadi wa Bokoli Jack Kawa naye kwa hafla hiyo amewataka wazazi ambao bado hawajafanikisha kupeleka wanao shuleni kujiunga na kidato cha kwanza kuwajibika ipasavyo ili kupunguza joto la visa potovu katika jamii ambavyo vinaweza shuhudiwa kufwatia ukosefu wa maadili mema.
I
"Kaunti ya Bungoma ndio ina asilimia kubwa ya watoto ambao bado kujiunga na kidato cha kwanza,tuangalie boma ambazo bado kupeleka watoto shuleni tuwasaidie na kama hatuwezi saidiana hao ndio watakuja kutusumbua baadaye", wito wa Kawa.
......kauli ya sauti iliyonaswa ipo.............
Uchapisho wake,
SIMIYU SAKWA-0702022524
Comments
Post a Comment