CHAMBUZI LA WIKI

GATUZI LA BUNGOMA:
WEBUYE MAGHARIBI
"HESHIMU UAMUZI WA MAHAKAMA:PALANG'A AMWAMBIA RAIS RUTO".
Mwakilishi wa wadi ya Olkaria,kaunti ya Nakuru Peter Palang'a amutaka Rais Dkt.William Ruto kuheshimu uamuzi wa mahakama kufwatia pendekezo la serkali ya Kenya kwanza la ujenzi wa nyumba za serkali
Palang'a anayewakilisha wakaazi wa Olkaria kwa hatamu ya nne kupitia kwa chama cha ODM,Kwenye hafla moja ya mazishi  ya mwalimu mstaafu Job Nakitare katika kijiji cha Sirandafu,kata ya Mahanga-Webuye magharibi,amesema Wakenya wengi wanapitia hali ngumu  kufwatia gharama za juu za maisha ikiwemo bei ya vitu vya matumizi ya kila siku kwa mwanainchi wa kawaida kupanda kila wakati.Aidha mtetezi huyo amesema ipo haja mbunge wa Webuye magharibi Dan Wanyama kuwajibika na kusemezana na Serkali kuu chini ya Wizara ya usafiri na uchukuzi kuafikia njia mwafaka ya makubaliano ili mwanakandarasi aliyepewa nafasi ya kukarabati barabara ya Sikata-Kimilili imalizike.
" Si ukumbushe Rais labda apeane pesa ya kumaliza hii barabara ya Khachonge hadi Kimilili", asema Palang'a.
.........kauli ya sauti iliyonaswa ipo......
Barabara ya Sikata-Kimilili  ilipendekezwa na serkali kuu kukarabatiwa na hali inayoshuhudiwa ni kwamba ukarabati ulifanywa kutoka maeneo ya sikata hadi kwa soko la Khachonge.Hali ambayo inazidi kuibua hisia tofauti huku  suluhisho likihitajika kushuhudiwa.
Palang'a,mzaliwa wa Bungoma  hakusita kusikitika kufwatia utendakazi wa baraza la mitihani humu nchini(Knec) kufwatia kucheleweshwa kwa matokeo ya mitihani ya kidato cha nne kwa shule  ya upili ya Wasichana ya Namawanga katika wadi ya Bokoli,huku akiomba ushirikiano wa Mbunge Wanyama na washikadau kutafuta sababu iliyosababisha matokeo hayo kuchelewa.
" Shule ya Namawanga ya wasichana,imefanya vizuri sana na ni lazima tuwashukuru lakini tena haya matokeo haikutoka mapema tulivyotarajia,na juzi wametangaza hayo matokeo wanafunzi wetu wakafurahi,lakini pia kama wakaazi tungependa kujua ni sababu gani ambayo ilikuwa imefanya hayo matokeo hayakutoka ndio kesho ingine isirudiwe",wito wa Palang'a
......kauli ya Sauti iliyonaswa ipo......
Naibu chifu wa Mahanga Festus Sangura akiomba wazazi kuhakikisha kila mtoto awe shuleni na kuwaomba kushirikiana na walimu kwa maadili bora ili kuzuia mimba za mapema kwa wanafunzi.Aidha mtawala huyo amesisitiza kuwepo haja kwa walio na ulemavu kujisajili katika hospitali ya kaunti- Kimilili na shillingi ksh.500 ili waweze kupewa vyeti miliki vitakavyowawezesha kupata huduma mbalimbali kiupesi.
Hafla hii ya mazishi ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali watawala na wanasiasa wakiongozwa na mbunge wa Webuye Maharibi Dan Wanyama na mwenzake kutoka nchi jirani ya Uganda Mheshimiwa Wandwasi.
Wanyama naye akipigia debe hoja ya serkali ya kubuni ujenzi wa nyumba kuwa mataifa ya kigeni yameendelea pakubwa kufwatia mipangilio kama hiyo ya ujenzi wa majumba huku akiwarai Wakenya kuwa na mtazamo wa pili kwa hilo swala.Aidha kusisitiza kuwa,japo wamekubaliana na uamuzi huo, demokrasia inawaruhusu kurudi mahakamani kuomba nafasi ya kupigia doria pendekezo hilo mradi wanaamini kama serkali litaafikia kusimamisha nchi kwa ustaarabu wa uchumi.
"Tuna uwezo wa kuheshimu uamuzi wa mahakama,tumesema ndio kama serkali lakini pia demokrasia  na sheria inaturuhusu kutetea pendekezo hilo kama tunaamini tukisema vyumba mashinani tuna mpango mzuri kwa watu wetu", asema mbunge Wanyama.
......Kauli ya Sauti iliyonaswa ipo....... 
Kilio cha wakaazi kufwatia  barabara ya Sikata-Kimilili,mbunge Wanyama alitumia fursa hiyo kuwahakikishia kuwa tayari amesungumza na waziri hitajika wa usafiri na uchukuzi Kipchumba Murkomen, kuwa kufikia katikati mwa mwezi wa Februari itakuwa imetengewa peza za kuendeleza ukarabati ili kukamilisha sehemu zilizobaki.
.......kauli ya sauti iliyonaswa ipo.....
 Uchapishaji wake,
  ...SIMIYU SAKWA...
<sakwasimiyu5.blogspot.co.ke>0702022524
BUNGOMA

Comments

Popular posts from this blog

UKATILI,BOKOLI-WEBUYE MAGHARIBI.

BUKUSU CULTURAL CENTRE

KUMWONJOLOLI KWE LIMENYA LIA KUKHU DINAH NAFULA MANYONGE.