NANI KAWA NYUMA YA HILI SWALA?

UHALIFU BOKOLI
Huku vitengo mbalimbali vya usalama pamoja na watawala wakipigana na visa vya uhalifu katika maeneo haya ambavyo mara nyingi inasemekana vinatokana na sherehe za utumbuizaji kwa matanga  wakati wa usiku(Disco-matanga),kitendawili hiki bado kupata kiteguo baada ya visa vingi vya uhalifu kuendelea kushuhudiwa katika wadi ya Bokoli.
Je,ni nani aliye nyuma ya visa hivi,na lengo ni lipi?
Wizi wa mifugo  unazidi kushuhudiwa katika maeneo haya licha ya utawala kutoa onyo kwa vijana wanao zurura usiku kuwa wakipatikana mkono wa sheria uko tayari kuwafungulia mashtaka.
Kisa kimoja mwaka jana baada ya kushuhudiwa katika eneo bunge la Kimilili ambapo kundi la watu wasiojulikana walivamia boma la mkaazi mmoja na kumuibia ng'ombe wake.Juhudi za kutafuta zilifua dafu baada ya ng'ombe yule kupatikana karibu na shamba lake kama amechinjwa huku baadhi ya sehemu za mwili zikikosekana.
Wakaazi wa wadi ya Bokoli katika kijiji cha Machakha A na Sikimbilo mtawalia wakishuhudisha kisa hicho,wakikosa kubaini ni lengo lipi la mifugo hawa kuibiwa na hatimaye kupatikana kama wamechinjwa huku baadhi ya sehemu za mwili zikikosekana.
               Picha ya ng'ombe-Machakha       
Ni swala ambalo limehitajika haki na doria kupigwa na vitengo vya usalamu kukomesha visa hivi vinavyozidi kufanya wanainchi wakikaa kwa hofu kufwatia hili swala,kuwa ni kisa cha tatu katika wadi hiyo kushuhudiwa.
Uchapisho wake Simiyu Sakwa
Webuye Magharibi.

Comments

Popular posts from this blog

BUNGOMA,HEALTH UPDATES

BUKUSU CULTURAL CENTRE

WANAMEME RECOGNIZED BY STATE