HISTORIA YA MAREHEMU ZAKAYO MILIMO TUMWA. 1.KUZALIWA Marehemu Zakayo alizaliwa mwaka wa 1982 akiwa mtoto wa pili wa Silas Tumwa(Mutecho)na Everlyne Nafula(Muliuli). KANISA Mwendazake Zake Zakayo Milimo alipokelewa katika matabau ya kanisa la marafiki mwaka wa 1984. ELIMU Mwenda zake Zakayo Milimo alianza elimu yake katika darasa la kwanza katika shule ya msingi ya Kitale stesheni mwaka wa 1987 hadi darasa la pili. 1994 alijiunga na shule ya msingi ya Bokoli Rc katika darasa la tatu na kusoma hadi darasa la name na kufanya mtihani wa kitaifa KCPE na kupita vizuri. Mwaka wa 2000 alijiunga na shule ya upili ya marafiki ya Mahanga katika kidato cha kwanza Hadi 2003 katika kidato cha tatu. Mwaka 2004 alijiunga na shule ya upili ya mtakatifu Maria-Bokoli katika kidato cha nne ambapo alikalia mtihani wa kitaifa wa sekondari KCSE. 2006 Alijiunga na taasisi ya kiufundi ya Matili na kusomea Ujenzi. TOHARI Marehemu alipaswa tohara mwaka wa 1996 akiwa Omusawa nambari 5. KAZI Mwenda zake aliaj...
Posts
Showing posts from March, 2025