UKATILI,BOKOLI-WEBUYE MAGHARIBI.
Familia moja katika kijiji cha Sango-Matunda Milani kata ya Bokoli,Webuye magharibi kaunti ya Bungoma inaomboleza kifo cha mwanao Peter Barasa wa darasa la pili katika shule ya msingi ya Sikimbilo baada ya mwili wake kupatikana kwenye shimo la choo huku sehemu za mwili zikiwa zimekatwakatwa. ( ILANI-PICHA HIZI NI ZA HOFU) sehemu za mwili wa mtoto,Peter Barasa baada ya kuondolewa kwenye shimo la choo. Ukizihitaji tuma ujumbe "picha"kwa whatsapp-0797272770 Akisungumza na kituo hiki mamake mzazi wa mtoto huyo wa miaka minane Bi Lindah Sangura,ameeleza kuwa tangu mwanawe kutoweka Siku ya Jumanne wiki Jana,alishikwa na masikitiko baada ya kupata ripoti kuwa mwili wa mwanawe umepatikana ndani ya choo. Mamake marehemu ambaye ni mjane,aliye na familia ya watoto 10,amesema licha ya mumewe kufariki na kumwachia uzao,hali ya mapato imekuwa ngumu kwenye upande wake ,hali iliyolazimu mzee Wanjala Sitini Kumuridhi,pasipokujua angeweza kutekeleza maafa haya. ...