Posts

Showing posts from May, 2024

ELIMU NA KILIMO,BUNGOMA

Image
ELIMU NA UCHUMI,WEBUYE MAGHARIBI. Tarehe 3 Mei 2024 Wito umetolewa kwa wanafunzi kujitenga na  visa vya tabia potovu ambazo zinaweza sababisha maisha yao kuzorota. Haya ni kwa mujibu wake mwalimu mkuu wa shule ya upili ya wasichana ya Lugulu Bi Dinah Cheruyoit kwenye hafla ya changisho iliyoandaliwa katika shule ya upili ya mtakatifu Anne Maloho wadi ya Bokoli-Webuye Magharibi. Cheruyoit aliyekuwa mgeni wa heshima katika hafla hiyo,alitumia fursa hiyo kuwataka wanafunzi kukomesha uhusiano wa mapenzi wakiwa wangali shuleni kama njia mojawapo ya kuzuia visa vya mimba za mapema.Aidha alisisitiza kuwepo haja ya wazazi kuwajibika kuendeleza elimu ya wanao katika vitengo mbalimbali baada ya kumaliza vidato vya nne ili kuwawezesha kujimudu mbeleni. "Kama uko na mtoto nyumbani hakufaulu kuingia chuo kikuu,wacha waingie vyule vya kiufundi vyenye serkali imeleta zenye zinawapa mpaka mikopo,hakuna kuhangaika wacha watoto wapate ujuzi na wajiunge na vikundi wajisajili serkali itawasaidia...