KIDOLE CHA LAWAMA:HOSPITALI YA BOKOLI
Hafla ya Mazishi ya Pamela Namulanda katika Kijiji cha Namilimo wadi ya Bokoli yakuwa uwanja wa kulekezea kidole cha lawama kwa usimamizi wa hospitali ya Bokoli.Marehemu aliaga baada ya madaktari kuzembea kumhudumia haraka wakati wakujifungua hali iliyosababisha maisha ya watu wawili kupotea.Madai mengineyo ni kuwa kuchelewesha kupewa rufaa ya kuenda Webuye kwa usaidizi ilisababishwa na ukosefu wa Ambulensi iliyokuwa imeenda Mjini Bungoma mafuta.Viongozi walalamikia swala hilo wakitaka huduma za matibabu ikiwemo upasuaji na Ubanuzi wa wodi kuimarishwa hospitalini humo. Jack kawa,mwakilishi Wadi ya Bokoli akisisitiza kuwa anaanzisha mkondo wa kubaini ni sababu gani Ambulensi hiyo haiwezi kuajibika huduma za watu wa Bokoli bali ni maswala mengineyo. Kawa alitumia hafula hiyo kuthibiti na kusema kina mama wasije kudanganywa kutozwa fedha iwapo wanazo kadi za Linda mama wakati wa kujifungua. Watahiniwa wa darasa la 8 mwaka huu waliopata alama 350 na juu waliombwa kutuma maomba yao ya kupat...